Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya ujumbe wa Ayatollah Alireza A'raafi, Mkurugenzi wa hawza, ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mvunja nguvu za madhalimu
Taifa kubwa na jasiri la Iran na mfumo wa fahari wa Jamhuri ya Kiislamu wamesimama imara juu ya ahadi yao kwa mashahidi jasiri na waadilifu wa muqawama, na wako bega kwa bega na majeshi ya ulinzi yaliyo na nguvu, ya kulipiza kisasi, huku wakimfuata Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Amiri Jeshi Mkuu katika kuulinda uhuru na utukufu wa nchi ya Kiislamu na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, na katika kuhifadhi damu safi ya mashahidi, kwa uthabiti kuliko wakati wowote watakuwa uwanjani.
Taifa letu makini katika nyakati za hatari na lahadha za kuamua hatima limekuwa mstari wa mbele kwa akili, mamlaka na ujasiri, na limeilinda nchi na malengo yake ya juu. Na sasa pia ni wakati wa kuwepo, kujitolea na kuwa macho, na kwa uhalifu na uchochezi wa adui madhalimu na Wazayuni kuzimwa, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, jawabu thabiti la Iran litakuwa ni lenye kuleta majuto.
Natoa pongezi na rambirambi juu ya kuuawa kishahidi kwa kundi la wananchi wapendwa, hasa makamanda na wakuu jasiri wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), na wa majeshi ya ulinzi, na wa Makao Makuu ya Majeshi yote, pamoja na kundi la wasomi na wanasayansi wa taifa la Kiislamu. Tunazitakia rehema nafsi zao safi, na tunaapa nao ahadi ya jihad na muqawama.
Wanazuoni wajuzi na hawza kama kawaida, pamoja na wananchi waaminifu na vijana jasiri, na muqawama, wanafanya upya ahadi yao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa Hujjatul Mahdi (aj), kwa mashahidi adhimu, kwa makamanda na wanasayansi waliouawa kishahidi, na wanasisitiza juu ya kusimama imara, muqawama na kulipiza kisasi dhidi ya maadui wakaidi na utawala wa Kizayuni. Pia wanawaita watu kuhudhuria katika sala za Ijumaa za kulipiza kisasi, mikusanyiko iliyotangazwa, na mkusanyiko wa fahari wa Ghadir Khumm, pamoja na mkusanyiko unaozunguka mhimili wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
“Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye, na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye huruma.”
Alireza A'raafi
Mkurugenzi wa Vyuo vya Dini
Maoni yako